Uchanganuzi wa mikakati wanayoitumia mapapasi katika kujifunza lugha ya pili mji mkongwe Zanzibar
Loading...
Date
2015
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Mapapasi ni watu wenyekumudu kuzungumza lugha mbalimbali za kigeni na kuweza kuzitumia kuwaongoza wageni, hata hivyo mikakati wanayoitumia katika kujifunza lugha hizo bado hazijatambulikana hivyo utafiti huu ulikuwa na madhumuni ya kutambulisha na kuainisha mikakati wanayoitumia mapapasi katikakujifunza lugha pia kuelezea jinsi mikakati hiyo ilivyowasaidia katika kujifunza lugha ya pili.Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Utabia ya Skinner ambapo katika nadharia hii nilitumia mhimili wa mazoezi,urudiaji na uigizaji pia nilitumia nadharia ya Muingiliano ya Long ambapo nilitumia mhimili wa kufanya mazoezi ya kuzungumza na wazawa wa lugha.Utafiti huu ulifanyika kisiwani Unguja katika sehemu ya Mji Mkongwe katika shehia ya Malindi,Shangani,Mkunazini na Forodhani.Utafiti huu ulikuwa ni wakwen da nyanjani na muongozo wa maswali ndio kilikuwa kifaa cha kukusanyia data. Mapapasi 16 katika 64 ndio waliohojiwa na wahojiwa hao walichaguliwa maksudi.Data iliyokusanywa ilikuwa ni mikakati wanayoitumia mapapasi katika kujifunza lugha ya pili pamoja na Maoni ya wasaiwa kuhusiana na mikakati wanayoitumia inavyowasaidia kujifunza lugha ya pili.Data ilichanganuliwa kwa kutumia vipengele;kufanya mazoezi ya kuzungumza na wazawa wa lugha,kufanya mazoezi ya mazungumzo baina ya mapapasi,kuwauliza maswali wanaojua lugha zaidi, kusoma vitabu,kutumia kamusi,kuhawilisha maarifa ya lugha ya kwanza,kutumia vyombo vya habari,kutumia mtandao,kujiunga na taasisi zinazofundisha lugha,kutumia vyombo vya teknolojia kama vile kanda za sauti na za kuonyesha na kufanya mazoezi zaidi.Utafiti huu utakuwa na mchango kwa watu wanaojifunza lugha ya pili na taasisi mbalimbali za kielimu.Vilevile utafiti huu utawanufaisha walimu, wanafunzi, watafiti wa lugha ya pili na jamii kwa ujumla.
ABSTRACT Beach boys are people who are able to speak different language in guiding tourist. Strategies they used are not well known by other people. The objectives of the study were to introduce and identify the strategies used by beach boys in learning second language. Also to explain and to asses how strategies they used help to learn second language. This study was guided by Behaviorist Theory of Skinner (1957) and Interaction theory of Long (1983).The data for this study were strategies used by beach boys and their views on how the strategies used help them on learning second language. The research technique used was interview and the data collected was analyzed qualitatively and quantitatively. This research is a contribution to second language acquisition (SLA) and is expected to benefit subsequent researchers in that area.
Description
Keywords
Lugha ya pili, Learning, Language, Zanzibar
Citation
Mohammed , M.H. (2015) Uchanganuzi wa mikakati wanayoitumia mapapasi katika kujifunza lugha ya pili mji mkongwe Zanzibar. Thesis (Masters). Islamic University in Uganda.